TSK

TSK · Yohana 6:39

Treasury of Scripture Knowledge references in Swahili NT.

Back to passage

"Msiogope, enyi kundi dogo! Maana Baba yenu amependa kuwapeni Ufalme.

Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,

Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta kwangu; nami nitamfufua mtu huyo Siku ya mwisho.

Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata.

Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.

(Alisema hayo ili yapate kutimia yale aliyosema: "Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja.")

Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kufuatana na kusudi lake.

Maana ninyi mmekufa na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: "Bwana anawafahamu wale walio wake," na "Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu."

Yuda 1:1 TSK

Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo.