TSK

TSK · Marko 13:22

مراجع Treasury of Scripture Knowledge في Swahili NT.

العودة إلى المقطع

"Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.

Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.

Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata.

Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: "Bwana anawafahamu wale walio wake," na "Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu."

Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha ninyi.

Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miujiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguni ushuke duniani mbele ya watu.