Mathayo 5:41
TSK
Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
TSK
مراجع Treasury of Scripture Knowledge في Swahili NT.
Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
Mtu asipochukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
"Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa "Sunagogi la Watu Huru", nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na walimu; miongoni mwao akiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.