TSK

TSK · 1 Yohana 4:21

Treasury of Scripture Knowledge references in Swahili NT.

Rudi kwenye kifungu

"Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.

Yesu akamjibu, "Ya kwanza ndiyo hii: Sikiliza, Israeli! Bwana Mungu wetu ndiye peke yake Bwana.

Nawapeni amri mpya: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda ninyi.

Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.

Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.

Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.

Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi.

Sisi tunajua kwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo na kuingia katika uzima kwa sababu tunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye na upendo hubaki katika kifo.

Na, amri yake ndiyo hii: Kumwamini Mwanae Kristo, na kupendana kama alivyotuamuru.