Kanuni ya Imani ya Kiorthodoksi

The Orthodox Creed

Kwa kweli tunamwamini Mungu mmoja, Mungu Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Tunamwamini Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, aliyezaliwa na Baba kabla ya nyakati zote. Nuru kutoka Nuru, Mungu wa kweli kutoka Mungu wa kweli; aliyezaliwa, si aliyeumbwa; mwenye asili moja na Baba; ambaye kwa yeye vitu vyote vilifanyika.

Kwa ajili yetu wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu alishuka kutoka mbinguni; akapata mwili kwa Roho Mtakatifu na kwa Bikira Maria, akawa mwanadamu.

Alisulubiwa kwa ajili yetu wakati wa Pontio Pilato, akateswa na akazikwa; siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu kama yasemavyo Maandiko.

Alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Baba yake; atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.

Naam, tunamwamini Roho Mtakatifu, Bwana na Mtoa uzima, anayetoka kwa Baba; ambaye pamoja na Baba na Mwana anaabudiwa na kutukuzwa; aliyenena kwa njia ya manabii.

Na Kanisa moja, takatifu, katoliki na la mitume. Tunakiri ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi.

Tunatazamia ufufuo wa wafu na uzima wa wakati ujao. Amina.